Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako, alitembelea banda la NSSF na kupata maelezo kutoka kwa Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele kuhusu ushiriki wa Mfuko katika Maonesho ya Wiki ya Vijana yanayoendelea Wilayani Bukoba Mkoani Kagera, ambapo Mfuko unatumia maonesho hayo kutoa elimu ya hifadhi ya jamii, kutambua na kuandikisha waajiri na wanachama kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kutatua kero za wanachama na kueleza fursa mbalimbali za Uwekezaji.
Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika banda la NSSF, walipatiwa elimu ya hifadhi ya jamii kuhusu umuhimu wa kujiunga na kujiwekea akiba. Utoaji wa elimu ya hifadhi ya jamii uliongozwa na Meneja wa NSSF Mkoa wa Kagera, Siraji Kisaki akisaidiana na baadhi ya wafanyakazi wa NSSF. NSSF ilishiriki Maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa kwa ajili ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kuandikisha wanachama, kusikiliza na kutatua kero pamoja na kueleza fursa mbalimbali zikiwemo za uwekezaji.

Kocha Shime autaka mchezo wa Colombia
Harmonize: Young Africans ni jeshi kubwa, hatupaswi kukata tamaa