Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Phillip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Tanzania yanayojulikana kama Swahili International Tourism Expo (SITE), jijini Dar es Salaam.

Maonesho hayo, yanayotarajia kufanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba 21 hadi 23, 2022 yamebeba kauli mbiu ya ‘Kuupeleka Utalii katika Ngazi za Juu (Taking Toursim to the New Heights).  

Akizungumzia maandalizi ya onesho hilo la sita kwa mwaka huu (2022), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Felix John amesema wadau mbalimbali wa nje na ndani watahudhuria na wanatarajia matokeo chanya katika kukuza Utalii wa Tanzania.

John ambaye aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, amesema, ‘’SiTE 2022 tumekuwa tukilisubiria kwa hamu, tangu kuahirishwa kwake mwaka 2019, na tunaamini vyombo vya habari vitasaidia kuhabarisha na kutangaza vivutio vilivyopo nchini.”

Harmonize: Young Africans ni jeshi kubwa, hatupaswi kukata tamaa
Malaria bado 'kaa la moto' nchini