Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kutumia fursa mbalimbali zilizopo nchini ikiwemo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kunufaika kiuchumi kupitia sekta hiyo. 

Dkt. Tax ametasema hayo alipokutana kwa mazungumzo na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya ASSECO  ya Poland, Adam Goral, inayojishughulisha na masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano yenye nia ya kuwekeza nchini.

Amesema, “Nia ya Serikali ya Tanzania ni kutaka kujiimarisha kwenye masuala ya Teknolojia ya Habari  na Mawasiliano (TEHAMA) ili kupitia teknolojia hiyo nchi iweze kunufaika kiuchumi.”

Dkt. Tax ameongeza kuwa, katika ulimwengu wa sasa mifumo mingi ya utendaji imebadilika ambapo kazi nyingi  hukamilishwa kwa kutumia vifaa vya kisasa kama simu, kompyuta na mtandao. Hivyo unahitajika uwekezaji wenye tija hususan kwenye eneo la usalama wa taarifa  za watumiaji.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax akiagana na Rais wa Kampuni ya ASSECO, Dkt. Goral.

Aidha, amesema, matumizi ya tehama nchini yameendelea kukua  siku hadi siku ambapo taasisi mbalimbali zikiwemo za Serikali, za Fedha, Shule, Hospitali na nyingine hutegemea teknolojia ya uhakika na salama ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na tija. 

Awali, akitoa mada kwenye mkutano huo kuhusu hali ya matumizi ya teknolojia ya habari nchini,  Mtaalam wa Tehama kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Brigedia Generali Mbaraka Mkeremy amesema Tanzania imepiga hatua katika matumizi ya tehama ambapo kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari hadi sasa watanzania wanaomiliki simu ni milioni 28 na muamala ya simu imeingiza mapato ya zaidi Shilingi Trilion 20 kwa mwaka 2021 pekee.

Majaliwa ampa mkandarasi siku 15 kukamilisha ujenzi
Magari matatu yagongana, mmoja afariki