Vyama vya upinzani nchini Uingereza vimetaka uchaguzi mkuu uitishwe, raia wamchague Waziri Mkuu mpya na kumaliza miezi kadhaa ya mvutano wa kisiasa nchini humo.

Hatua hiyo, inakuwa wakati ambapo wagombea wanaowania uwaziri mkuu wa Uingereza kufuatia hatua ya Liz Truss kujiuzulu jana (Oktoba 20, 2022), wakitarajiwa kuanzisha kampeni za kutafuta uungwaji mkonokuanzia hii leo Oktoba 21, 2022.

Viongozi wa kisiasa nchini Uingereza. Picha: The Telegraph

Miongoni mwa wanaopigiwa upatu kuwania wadhifa huo, ni waziri mkuu wa zamani ambaye pia aliondolewa madarakani Boris Johnson na Rishi Sunak aliyeshindwa na Truss katika kinyang’anyiro kilichopita.

Wachambuzi wa siasa nchini humo wamesema, chama cha Conservative kinapaswa kumpata kiongozi atakayekiunganisha chama badala ya kukigawa na Truss alijiuzulu baada ya kukaa madarakani kwa siku 45 kufuatia mpango wake wa kiuchumi kusababisha mtikisiko katika masoko ya fedha.

Kagera Sugar yahamishiwa CCM KIRUMBA
Simba Queens yapongwezwa, kuanza safari ya Morocco