Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amewataka Waandishi wa habari nchini kujikita katika uandishi wa Habari zinazotetea taaluma na maslahi yao.

Balile, ametoa wito huo Jijini Dar es Salaam wakati wa semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na jukwaa hilo kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu utetezi wa mabadilko ya Sheria ya vyombo vya habari.

Amesema, “Waandishi wa habari wana jukumu kubwa la kutetea taaluma yao na maslahi yao kwa ujumla lakini zipo baadhi ya sheria zinasababisha kushidwa kufanya kazi zao kwa weledi na hivyo kushidwa kutetea haki na maslahi yao.”

Balile pia amezengumzia vifungu vya sheria ya habari, na kusema tayari vipo katika mchakato kuona namna ambavyo Bunge litapitia upya sheria hizo hasa zinazoleta vikwazo kwa waandishi wa habari ili vifanyiwe marekebisho.

Kwa upande wake, Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Dkt. Wiebe de Boer amelipongeza Jukwaa la Wahariri (TEF), kwa kuwa na programu za kuwajengea uwezo wanahabari, ili wafanye kazi kwa weledi na kusema wapo tayari kutoa ushirikiaono.

EU wafikia makubaliano bei ya nishati
GGML, Rafiki Surgical Mission watoa ‘Ambulance’ mbili Geita