Mwenyekiti wa kikosi kazi cha wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa, Profesa Rwekaza Mkandala Awali, ametaka Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), isilazimike kufuata amri au maelekezo ya mtu yoyote wa Serikali, maoni yoyote ya chama cha Serikali, taasisi au asasi yoyote na kwamba utendaji wake uruhusiwe kuhojiwa katika Mahakama kuu ili kuongeza uwajibikaji.

Mukandala ameyasema hayo hii leo Oktoba 21, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha taarifa ya kikosi kazi cha wadau wa Demokrasia ya vyama vingi vya siasa na kubainisha dhamira ya utawala wake kutaka kuwa na mazingira mazuri ya kuendesha shughuli za kisiasa nchini.

Mwenyekiti wa kikosi kazi cha wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa, Profesa Rwekaza Mkandala akimkabidhi Rais Samia Suluhu Hassan, taarifa ya kikosi kazi cha wadau wa Demokrasia ya vyama vingi vya siasa.

Aidha, pia Mukandala aliibua hoja ya katiba mpya na kupendekeza mchakato wake uanze mara moja baada ya kukamilika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, huku suala hilo likikosa majibu ya moja kwa moja wakati Rais Samia akijibu mambo machache kati ya hayo.

Hata hivyo, chama kikuu cha upinzani CHADEMA ni miongoni mwa makundi ambayo yalisusia kujumuishwa na Rais Samia wakati wa kuundwa kwa kikosi hicho, huku akisema bado ataendelea na mazungumzo na makundi ya namna hiyo ili yaweze kujumuishwa.

Urusi, Ukraine zajipanga na mashambulizi mapya
Boris autamani tena uwaziri Mkuu, apingwa