Viongozi wa Umoja wa Ulaya EU, wamekutana jijini Brussels kwa mkutano wa kilele wa siku mbili ulioanza hapo jana Oktoba 20, 2022 wa kujadili vita vya Ukraine na mzozo wa nishati.

Viongozi hao, wanatarajiwa kulijadili kwa kina suala la kupunguza bei ya nishati katika ukanda mzima licha ya uwepo wa mgawanyiko miongoni mwa nchi wanachama juu ya ukomo wa bei ya gesi.

Moja ya mikutano ya Viongozi wa Ulaya. Picha: Olivier Matthys /AP

Ufaransa na Poland ni miongoni mwa mataifa 15 yanayounga mkono hoja ya kuwepo na ukomo katika bei ya gesi, wakati Ujerumani na Uholanzi zikipinga hatua hiyo.

Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Charles Michel hii leo Oktoba 21, 2022 amesema wataendelea kufanya kazi ili kukabiliana na mgogoro wa nishati ndani ya muungano huo, ulioachangiwa na vita vya Ukraine.

Rais Samia apokea ripoti ya Kikosi kazi Demokrasia
U-23 kuikabili Nigeria Kwa Mkapa