Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suhulu Hassan amepokea taarifa ya kikosi kazi cha wadau wa Demokrasia ya vyama vingi vya siasa na kubainisha dhamira ya utawala wake kutaka kuwa na mazingira mazuri ya kuendesha shughuli za kisiasa nchini. 

Rais Samia ameyasema hayo hii leo Oktoba 21, 2022 jijini Dar es Salaam, na kusema ni matamanio yake kuona Tanzania inaendelea kuwa moja na salama bila ya kuwa na kundi litakalohisi kuachwa nyuma katika ufurahiaji wa demokrasia ya kweli..

Amesema, “Kuna ambayo ni mepesi tunaweza kuyafanyia kazi haraka, lakini kuna yale ambayo lazima tukae na kuangalia sheria zilizopo zina mapungufu wapi? Na tunayabadilisha vipi kutokana na maoni yenu.”

Aidha, amewataka wajumbe wa kikosi hicho kutafakari namna ya kuwasilisha ripoti itakayozitafutia majawabu changamoto hizo, na kwamba nyingine zitapata ufumbuzi wa haraka hata kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024.

Tshabalala: Wao wenyewe watashangaa
Majadiliano ukomo bei ya Nishati yapamba moto