Wanajeshi wa Urusi na Ukraine, wanajiandaa kwa mapambano makali katika mji wa kimkakati wa Kherson, huku mapigano na uhamishaji wa raia vikiripotiwa katika mkoa huo.

Hata hivyo, wakati taarifa hiyo ikijiri bado Wanajeshi wa Urusi wanaendeleza mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya miundombinu muhimu ya Ukraine.

Maafisa wa Urusi wameswema kwamba raia elfu 15,000 kati ya 60,000 tayari wamehamishwa kutoka mji huo na maeneo ya jirani ambapo Rais wa Urusi, Vladimir Putin alitangaza sheria ya kijeshi katika mikoa ya Kherson, Luhansk, Donetsk na Zaporizhzhia.

Tangazo hili ni jaribio la kusisitiza mamlaka ya Urusi katika maeneo hayo huku vikosi vya Ukraine vikidai kufanya mashambulizi 15 kwenye ngome za kijeshi za Urusi katika mkoa wa Kherson na wizara ya ulinzi ya Urusi nayo ikisema imezuia jaribio la vikosi vya Ukraine kusonga mbele katika mkoa huo.

Makamba azitaja EWURA, NEMC utitiri vituo vya mafuta
Mukandala ataka utendaji wa NEC uhojiwe