Kiongozi wa mrengo wa kulia nchini Italia, Giorgia Meloni amehimizwa kuchukua hatua madhubuti ili kukabiliana na majanga yaliloyakumba Mataifa mengi la ukali wa maisha na kuyumba kwa uchumi.

Meloni anakutana na ujumbe huo mara baada ya kula kiapo kuwa Waziri Mkuu wa Italia na kuahidi kufanya kazi kwa karibu na washirika wake wa kimataifa, licha ya mitazamo tofauti ya washirika wake wa muungano.

Kiongozi huyo ambaye ni mwanamke wa kwanza kuongoza serikali ya Italia, aliapishwa mbele ya Rais Sergio Mattarella katika Ikulu ya Quirinal huko Roma, huku Viongozi mbali mbali duniani wakimtumia salamu za pongezi.

Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni. Picha: WIEN

Rais wa Halmashauri kuu wa Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen naye amempongeza Meloni na kusema anategemea kupata ushirikiano wa maendeleo na serikali hiyo mpya, katika changamoto zinazowakabili.

Akijibu ujumbe wa pongezi kutoka kwa katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami ya NATO, Jens Stoltenberg Meloni amesema yupo tayari kushirikiana na NATO ambayo ni zaidi ya muungano wa kijeshi na ngome ya maadili ya pamoja.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Octoba 24, 2022    
Wadau wa Habari wapongeza kauli ya Mukandala