Wananchi wa Mkoa wa Iringa, wametakiwa kushirikiana na mamlaka husika za Serikali ili kudhibiti matukio ya moto ambayo yamekuwa yakijitokeza kwenye mashamba ya miti binafsi na ya Serikali.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja wakati wa ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta katika Shamba la Miti Saohill, Kijijini Kibengu Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.

Amesema, “Niwaombe sana kila mtu awe mlinzi wa mwenzie, kama unaandaa shamba hakikisha unaangalia upepo unaelekea wapi ndipo uchome ili kuepusha madhara.

Aidha, Naibu Waziri Mary pia amewaomba wananchi kuwasiliana na viongozi kipindi wanapoanza kuandaa mashamba yao, ili waweze kuwa karibu na kudhibiti moto unaoweza kujitokeza.

Hata hivyo, amesema mashamba ya miti yamekuwa msaada mkubwa kwa wananchi kwa kutoa ajira, kama ilivyo kwa Shamba la Miti Saohill, ambalo limeajiri zaidi ya watu 4000.

Juma Kaseja atangaza kutundika GLOVES
Putin ajipanga na shambulio la nyuklia