Rais wa Iran Ebrahim Raisi ameapa kujibu vikali shambulizi lililosababisha vifo vya karibu watu 15 lililofanywa kwenye eneo muhimu la ibada la waumini wa Shia nchini Iran.

Kundi la wanamgambo linalojiita Dola la Kiislamu limekiri kuhusika na shambulizi hilo, na kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi ya Raisi imewalaani aliowaita ‘maadui wa Iran wanaojaribu kuligawa taifa hilo kwa kutumia machafuko na ugaidi.

Katika shambulio hilo, watu 19 walijeruhiwa wakati wa ibada ya jioni kwenye eneo la makaburi la Shah Cheragh katika jiji la Shiraz.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Hossein Amirabdollahian amesema Iran haitanyamazia shambulizi hilo na kuonya hawataruhusu usalama na maslahi ya Iran kuchezewa na aliowataja kuwa ”magaidi na wavamizi wa kigeni wanaodai kutetea demokrasia”.

DC, Wakurugenzi kusimamia sheria udhibiti ulevi
U20 CECAFA: Ngorongoro Heroes yaenda Sudan