Suala la ukosefu wa ajira na usawa linaendelea kushika kasi Ulimwenguni, kutokana na majanga mbalimbali yanayoingiliana kiuchumi na kisiasa na hivyo kutishia ukwamuaji wa soko nanupataji wa maendeleo.

Hayo yamebainishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani (ILO), kupitia ripoti yake iliyotolewa mjini Geneva, Uswisi ikionesha mwelekeo mbaya wa soko la ajira duniani katika miezi ya hivi karibuni na kupungua kwa nafasi za ajira.

Ripotinhiyo, imeeleza kuwa kiwango cha ukuaji wa ajira duniani kwenye robo ya mwisho ya mwaka huu wa 2022 iliyoanza mwezi huu wa Oktoba kimeshuka na kwwmba juhudi za dhati zinatakiwa kuchukuliwa ili kudhibiti hali hiyo.

Binti aliyeamua kujiajiri. Picha: UN

Kuhusu ufuatiliaji wa Sekta ya Ajira duniani, ripoti hiyo imezidi kueleza kuwa inasema vita ya Ukraine, pamoja na ongezeko la mfumuko wa bei vinasababisha kuporomoka kwa viwango halisia vya ujira kwenye nchi nyingi duniani, ikiambatana na kuporomoka kwa ujira wakati wa janga la Uviko-19.

Hata hivyo, ukosefu wa ajira unadhihirika zaidi kupitia madhara yake kwenye ongezeko la bei za vyakula na nishati, uchumi kuadorora na kupungua kwa fursa za maboresho ya kisera.

Mkurugenzi Mkuu wa ILO, Gilbert Houngbo anasema ili kupata majawabu ya utatuzi wa hali ya sasa ya ajira, kutahitaji utekelezaji wa sera za kina zinazoingiliana na mizania kitaifa na kimataifa.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 2, 2022     
Korea Kaskazini ‘yaipiga stop’ Marekani