Mamlaka ya usalama Korea Kaskazini, imeitaka Marekani na Korea Kusini kuachana na luteka kubwa za pamoja za kijeshi, ikisema huo ni uchokozi unaoweza kuchochea hatua kali zaidi kutoka kwa Pyongyang. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini, imesema hali katika rasi ya Korea na viunga vyake kwa mara nyingine imeingia katika awamu ya kupambania mamlaka kutokana na harakati za kijeshi za Marekani na Korea Kusini.

Kikosi cha kijeshi nchini Korea ya Kaskazini. Picha: South China Morning post.

Mapema hivi karibuni, Marekani na Korea Kusini zilianza luteka kubwa za kijeshi na hapo Jumatatu Oktoba 31, 2022 zinajumuisha upitishaji na safari za anga za takriban ndege 240 za kivita utakaoendelea hadi siku ya ijumaa Novemba 4, 2022. 

Hata hivyo, Marekani na Korea Kusini wanaamini kwamba Korea Kaskazini huenda wakaanzisha tena majaribio ya makombora ya nyuklia, yaliyofanyika kwa mara ya mwisho mwaka 2017, wakijiandaa kulidhibiti taifa hilo kupitia mazoezi ya kijeshi.

Ukosefu wa ajira ‘bomu jipya’ Ulimwenguni
Rais Samia ampa mwaka mmoja Waziri Makamba