Aliyekuwa Afisa Habari wa Young Africans Hassan Bumbuli ametoa maoni yake kwa uchungu kuhusu mwenendo wa Klabu hiyo katika Michuano ya Kimataifa, baada ya kuambulia sare ya bila kufungana jana Jumatano (Novemba 02) dhidi ya Club Africain ya Tunisia.
Young Africans ilicheza mchezo huo wa Mkondo wa Kwanza hatua ya mtoano Kombe la Shirikisho Barani Afrika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, na sasa inajipanga kwenda Tunis-Tunisia kucheza mchezo wa Mkondo wa Pili Jumatano ijayo (Novemba 09).
Bumbuli ametoa maoni yake kwa kuandia makala katika Mitandao ya Kijamii akianza na Kichwa cha Habari, TUMEHUZUNIKA
Matokeo ya leo (jana) yametuhuzunisha, huzini imeongezeka mara dufu kutokana na makelele na vicheko vya Watani zetu.
Wanatucheka, wanatusema, wanatutambia! Ni haki yao, kwani kwa hakika wao wanarekondi nzuri na Bora zaidi kuliko sisi kwenve michuano ya kimataifa.
Wanarekodi ya kucheza Fainali ya Kombe la CAF (Sasa Shirikisho)1993. Na misimu hii mitatu kuanzia 2020/21 hadi leo, watani wameshinda mechi 5 kati ya 14 za Kimataifa akiwa ugenini (As Vita, Plateau, Galaxy, Nyasa, Agusto).
Kwenye uwanja wa Nyumbani wao wanatamba sana wameshinda mechi 13 kati ya 14, kati ya hizo wameshida mechi 6 za group stage na mbili za Robo Fainali.
Hatuna cha kuwatambia kwenye hili, sisi katika mechi 13, tumeshinda mechi 3 tu, ugenini 2 (Township na Zalan) na kupoteza 6, nyumbani tumeshinda mechi 1 (Zalan), tumefungwa 2 (Pyramids, Rivers) na sare 4 (Township, Zesco, Hilal na African).
Acha watucheke, wanayo sababu ya kutucheka, vicheko vyao vitufanye tutafute maarifa zaidi ya kufanya vizuri ili kuzima kelele za vicheko vyao.