Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila amesema Ndege ya Precision Air iliyopata ajali wakati wa kutua Bukoba leo ilikuwa imebeba Watu 43 ambapo hadi sasa wameokolewa 26 tu na kupelekwa hospital ya Rufaa ya mkoa Kagera.
“Tuna mawasiliano na walioko majini na juhudi za uokozi zinaenda vizuri. Tuna bahati ni ziwa na angalau tumeweza kuwaona hao waliookolewa tayari vinginevyo tungekuwa tunaongea habari nyingine,” alisema Chalamila.