Kikosi cha Simba SC kimewasili salama jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa Mzunguuko wa 16 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Geita Gold FC.

Simba SC itakayokuwa mgeni wa mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba Jumapili (Desemba 18), ilianza safari mapema asubuhi, ikitokea jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Kurasa za Mitandao ya Kijamii ya Simba SC, Kikosi cha Simba SC kimewasili salama jijini Mwanza, huku wachezaji waliosafiri na timu wakionesha kuwa na furaha.

Mashabiki na Wanachama wa Simba SC wa jijini Mwanza wamejitokeza Uwanja wa Ndege jijini humo kuipokea timu yao, ambayo itaendelea kuwa Kanda ya Ziwa hadi mwishoni mwa mwezi huu.

Baada ya kucheza dhidi ya Geita Gold FC Jumapili (Desemba 18), Simba SC itaelekea mkoani Kagera kucheza dhidi ya Kagera Sugar siku ya Jumatano (Desemba 21) na baadae itarejea jijini Mwanza kuikabili KMC FC Desemba 26 katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Ugonjwa wa ajabu waisumbua Ufaransa
Lionel Messi: Alvares ametufikisha hapa