Mshambuliaji na Nahodha wa Kikosi cha Argentina Lionel Messi amekiri kuvutiwa na uwezo wa Mshambuliaji Julian Alvarez, kwa kusema amekua msaada mkubwa wa Taifa hilo, tangu walipoanza kupambana na kufika hatua ya Fainali.

Jumapili (Desemba 18) Argentina itacheza dhidi ya Ufaransa katika mchezo wa Fainali wa Michuano ya Kombe la Dunia iliyoendelea nchini Qatar.

Messi amesema Alvares amekua na kiwango cha kustaajabisha, na hilo halijatokea kwake kama mchezaji mwenzake, bali anaamini hata kwa Mashabiki wamekua wakishangazwa na uwezo wake.

“Hakuna aliyefikiria Julian angekuwa msaada mkubwa katika kikosi cha Argentina, ameonesha uwezo mkubwa na kutufikisha hapa,”

“Kiwango kikubwa alichokionesha kimekua msaada mkubwa kwa timu, naamini pia kimewashangaza Mashabiki wengi duniani.”

“Amekuwa na Kiwango Bora tangu tulipoanza safari yetu na kufika Fainali tukiwa hapa Qatar, naamini hata mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Croatia Mashabiki waliendelea kushangazwa na kiwango chake,”

“Amekua akijitoa kwa hali zote anapokuwa na mpira na hata asipokuwa mpira, kwa hakika ni mchezaji wa aina tofauti kabisa, Binafsi ninamshukuru na nitaendelea kumshukuru kwa mazuri aliyotupa kwenye kikosi chetu cha Argentina, anastahili kitu mwishoni mwa Fainali hizi.” amesema Messi

Kwa mara ya kwanza Alvarez ambaye ni mchezaji wa Manchester City ya England, alianza kuitumikia Timu ya Taifa ya wakubwa ya Argentina mwaka 2021, na ameshafunga mabao saba katika michezo kumi na nane aliyocheza.

PICHA: Simba SC yawasili salama Mwanza
Real Madrid yanasa Kinda la Kibrazil