Kalbu ya Arsenal imeonywa kwamba isithubutu kuleta janga kwa kumsajili Cristiano Ronaldo eti kwa sababu tu anapatikana bure.

Ronaldo, 37, ametemwa na klabu yake ya Manchester United baada ya kufanya mahojiano na Piers Morgan, ambaye ni shabiki mnazi wa klabu ya Arsenal. Katika mahojiano hayo, Ronaldo aliwashutumu mabosi wa Man United, huku akitangaza hadharani kwamba hawezi kumheshimu kocha Erik ten Hag.

Piers atapenda kuona Ronaldo anajiunga kwenye kikosi cha Arsenal hasa ukizingatia saini yake ni ya bure kabisa. Lakini, beki wa zamani wa Arsenal, Nigel Winterburn amewaonya mabosi wa klabu hiyo wasithubutu kabisa kumvuta staa huyo huko Emirates.

“Kwangu mimi hapana na sababu ni rahisi tu, unaziba pengo la muda mfupi. Kuna watu wanasema safi, tumsajili tu.”

“Mimi nisingeruhusu, ukitazama namna Arsenal ilivyoanza kucheza mechi zao, wanaanza kukaba kuanzia juu, sawa Ronaldo ni mchezaji mzuri, lakini sidhani kama ana nguvu tena za kufanya kama washambuliaji wa Arsenal wanavyofanya.”

“Kama Arsenal wanahitaji kubadili staili yao ya uchezaji basi wamchukue. Lakini, mimi ninachokiona itakuwa majanga makubwa.”

Azam FC kuvaa Jezi Nyeusi Desemba 25
Ajibu asaini miwili Singida Big Stars