Afisa Habari wa Azam FC Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ ameibua mjadala mzito katika Mitandao ya Kijamii, kuhusu matarajio ya Kikosi chao kuvaa Jezi Nyeusi wakati mchezo wa Mzunguuko wa 18 wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaowakutanisha dhidi ya Young Africans.

Mchezo huo utashuhudia Azam FC wakiwa ugenini Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili (Desemba 25), huku Young Africans wakiendelea kuwa nyumbani baada ya kufanya hivyo katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union.

Zaka Zakazi ambaye kwa sasa anatumikia adhabu ya kufungiwa na TFF, amesisitiza kuwa Kikosi chao siku hiyo kitavaa Jezi Nyeusi ili kuwaenzi Wadhamini wao Azam Max.

“Siku ya Krismasi (Kwenye Mechi yao dhidi ya Yanga) tutavaa jezi zetu NYEUSI katika mchezo wetu wa nyumbani dhidi ya Yanga.Tutavaa jezi nyeusi ili kumuenzi Mdhamini wetu AZAM MAX”

Hata hivyo mjadala huo unaoenakana kuleta mkanganyiko kwa Mashabiki wa Young Africans, ambao wamekuwa na imani za kupata alama tatu kwa uhakika endapo timu yao inavaa Jezi Nyeusi inapocheza Nyumbani ama Ugenini.

Lakini pamoja na mjadala huo kuwa mzito Mitandaoni, Uongozi wa Young Africans haujasema lolote hadi sasa, licha ya Kanuni kuwa wazi kwa timu mwenyeji kutakiwa kuvaa Jezi za Nyumbani inapokua katika Uwanja wake.

Mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza wa Ligi Kuu uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa na kumalizika kwa sare ya 2-2, Azam FC ilivaa Nyeusi huku Young Africans ikivaa Jezi za Kijani.

PICHA: Mashujaa wa Afrika wapokewa kishujaa
Cristiano Ronaldo akataliwa Arsenal