Licha ya kumaliza nafasi ya nne katika Fainali za Kombe la Dunia, Kikosi cha Morocco kimepokewa kishujaa baada ya kurejea nyumbani katika mji wa Rabat.

Morocco iliyokua haipewi nafasi ya kufanya vizuri miongoni mwa Mataifa ya Afrika yaliyoshiriki Fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, ilicheza mchezo wa Mshindi wa Tatu dhidi ya Croatia na kupoteza kwa 2-1.

Kabla ya hapo Morocco iliishangaza Dunia kwa kuiondoa Hispania katika mchezo wa 16 Bora, kisha ikaifunga Ureno kwenye Hatua ya Robo Fainali kabla ya kukwama Hatua ya Nusu Fainali kwa kufungwa na Ufaransa mabao 2-0.

Kitendo hicho cha kupambana na kuweka Rekodi mpya na kuwa timu ya Kwanza ya Afrika kufika Hatua ya Nusu Fainali, kimekua chagizo kwa Mashabiki wa soka na Viongozi wa Serikali nchini Morocco kujitokeza kwa wingi kukilaki kikosi chao kilipowasili mjini Rabat.

Wazazi wakutana kwa Mfalme Mohamed VI
Azam FC kuvaa Jezi Nyeusi Desemba 25