Mkuu wa Mahakama ya Juu ya Ethiopia, Meaza Ashenafi, na naibu wake, Solomon Areda Waktolla wamejiuzulu wadhifa wao.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Addis Standard liliripoti january 17, kuwa Barua iliyotumwa kwa Baraza la Wawakilishi wa Watu (HoPR) haikutaja sababu ya kujiuzulu.
Ambapo, baadaye Bunge limeidhinisha Msaidizi wa Profesa Tewdros Mihret, kutoka chuo kikuu cha Addis Abeba kuwa Jaji Mkuu, na Jaji wa Mahakama ya Juu ya Shirikisho, Abeba Embiale, kuwa Naibu Jaji Mkuu akichukua nafasi za Meaza na Solomon mtawalia.
Jaji Mkuu Meaza na naibu wake Solomon walipendekezwa na Waziri Mkuu Abiy Ahmed kwenye Baraza la Wawakilishi wa Watu (HPR) Tarehe 01 Novemba 2018. ambapo wote wawili wamepokea kura kwa kauli moja kutoka kwa Baraza hilo.
Solomon hivi karibuni ameteuliwa kuwa jaji wa muda wa Mahakama ya Mizozo ya Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha 2023-2030 na mkutano wa 34 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika uchaguzi uliofanyika tarehe 15 Novemba 2022 mjini New York.