Kikosi cha Klabu Bingwa nchini Ufaransa PSG kimewasili mjini Doha kwa ziara, ambapo inatarajiwa kucheza michezo ya kirafiki na kikosi cha wachezaji wa ligi ya Saudi Arabia ‘Saudi All Stars Team’, Januari 19, 2023.

Cristiano Ronaldo ambaye anakipiga katika klabu ya Al Nassir ya Saudi Arabia, amejumuishwa katika kikosi cha ‘Saudi All Stars Team’ kitakachocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya PSG inayotumikiwa na nyota wa Argentina, Lionel Messi.

Mara ya Mwisho Messi na Ronaldo kukutana uwanjani ilikuwa ni msimu wa mwaka 2020/21 kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa Barani Ulaya Hatua ya Makundi, FC Barcelona dhidi ya Juventus ambapo Ronaldo alifunga magoli mawili ya Penati katika ushindi wa magoli 3-0 walioupata Juventus katika Dimba la Camp Nou.

Kikosi cha PSG pia kinamjumuisha Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe pamoja na Beki wa Kulia Achraf Hakimi, ambao kwa pamoja walikuwepo nchini Qatar wakati wa Fainali za Kombe la Dunia 2022, zilizounguruma kuanzia Novemba 18 hadi Desemba 20, 2022.

Ronaldo kuingoza Saudi All Stars
Mkuu wa Mahakama ya Juu ajiuzulu