Aliyekuwa Afisa Habari wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Hassan Bumbuli, ameingilia kati suala la ujio wa Kocha Msaidizi mpya wa Simba SC Ouanane Sellami, ambalo linahusishwa na kuondoka kwa Kocha Msaidizi Mzawa Juma Mgunda.

Simba SC ilimtangaza Ouanane Sellami jana Alhamis (Januari 19) majira ya jioni, ambaye anaungana na makocha wengine klabuni hapo kwa ajili ya kuongeza ujuzi wa kukinoa kikosi cha Msimbazi.

Bumbuli ameingilia suala hilo, kwa kuchapicha taarifa maalum katika kurasa zake za Mitandao ya Kijamii, akipinga Propaganda zinazoendelea kusambazwa kwa makusudi, na baadhi ya watu ambao anaamini wamedhamiria kumuondoa katika malengo Juma Mgunda.

Bumbuli amemtaka Juma Mgunda kupuuza kinachoendelea Mitandaoni na badala yake achape kazi kwa maslahi ya kuisaidia Simba SC kufanya vizuri katika Michezo ya Ligi Kuu na Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Hatua ya Makundi.

Bumbuli ameandika: Juma Mgunda piga kazi

Objective Jounalism imekuwa changamoto kubwa kwa waandishi wengi wa habari za michezo hapa Tanzania. Sijui tatizo ni nini?

Wengi tumechagua kuchapisha taarifa za taharuki na unbalanced na pengine purpose edit ili mradi tusomwe na tuvuti watu kwenye kurasa zetu za Social Media.

Mifano iko wazi na dhahili, kwa mfano waandishi wanafahamu kabisa kwamba mabadiliko ya mfuko kwenye soka la kisasa yaliondoa neno KOCHA MSAIDIZI KWA UJUMLA WAKE kwa kuwa kuna spcializations kadhaa za makocha, hivyo kuna kuwa na kocha Mkuu (In charge/Manager) then kuna kuwa seti ya wasaidizi kulingana na uwezo wa klabu.

Mkanganyiko ulioibuka baada ya Simba kutangaza kocha msaidizi kama waandishi tungefanya kazi yetu ipasavyo leo isingekuwa mjadala. Kwa kuwa Kocha Mkuu ni mmoja wengine wote wanakuwa wasaidizi kulingana na maeneo yao kucheza mpira, Viungo, makipa, washambuliaji, utimamu wa mwili, phycology nk. Klabu kubwa zina seti ya makocha wasaidizi wengi zaidi ya sisi hapa.

Hata kwenye taaluma yetu ya Habari Mhariri Msaidizi wa jumla iliondoka kutokana na mahitaji ya mabadiliko ya mfumo, sasa kuna Mhariri Mkuu then kuna seti ya Wahariri (Wasaidizi) kulingana na vitengo, Habari, Makala, Uchumi, Siasa, Michezo nk ambao tunawaita Section Editors.

Juma Mgunda piga kazi.. IJUMAA KAREEM

Ahmed Ally: Tumefurahia maamuzi ya Kocha
Shinyanga kuondokana na changamoto maji safi na salama