Klabu ya Arsenal ipo kwenye mazungumzo na Uongozi wa Brighton ili kuangalia uwezekano wa kumsajili Mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji Leandro Trossard.

Arsenal wameingia kwenye mpango huo, baada ya kushindwa kukamilisha dili la Mykhailo Mudryk aliyetimkia Chelsea, juma lililopita.

Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa The Gunners bado hawajaweka wazi Ofa ya usajili wa Mshambuliaji huyo, lakini wameonesha dhamira ya dhati ya kutaka dili hilo likamilishwe kipindi hiki cha Dirisha Dogo.

Pamoja na yote hayo, Uongozi wa Brighton mwishoni mwa mwaka 2022 uliwahi kusisitiza kuwa, hautamuuza mchezaji yoyote wakati wa Dirisha Dogo la Usajili, kutokana na mipango na mikakati ya kuhakikisha wanaendelea kuwa na kikosi imara msimu huu.

Tayari Klabu hiyo imeshaikataa ofa ya Tottenham iliyokuwa imemlenga Trossard, na badala yake Spurs imebadilisha mpango na kuanza kumfuatilia Nicolo Zaniolo wa AS Roma ya Italia.

Trossard amebakisha mkataba wa miezi sita huko Brighton, lakini Seagulls wamedhamiria kumuongeza mkataba mpya.

Serikali yatoa kipaumbele kugharamia miradi ya maji
Ujerumani yapanga kurejesha mafuvu ya vichwa Afrika Mashariki