Mshambuliaji kutoka DR Congo na Klabu ya Young Africans amewashusha ‘PRESHA’ Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo, kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika Jumapili (Februari 12).

Young Africans itacheza dhidi ya US Monastir itakayokuwa nyumbani, Uwanja wa Hammadi Agrebi, Tunisia majira ya saa moja usiku kwa saa za Tanzania.

Mayele ambaye ni Mshambuliaji tegemeo katika kikosi cha Young Africans amesema, mchezo dhidi ya US Monastir utakua mgumu sana, lakini wamejipanga kupambana ili kupata matokeo mazuri.

Amesema Wachezaji wenzake wameonesha kuwa tayari kuipigania timu yao, ambayo ina ubora wa kupambana popote Barani Afrika.

“Tuna mchezo mgumu sana, lakini sisi kama wachezaji ni wajibu wetu kuingia uwanjani, na kuipambania timu ili kupata matokeo mazuri,”

“Tuna ubora ambao unatufanya tuwe na uwezo wa kupambana popote, ndio maana tupo huku Tunisia kwa ajili ya kupata matokeo mazuri na wala sio kuushangaa mji na majengo yake.” amesema Mayele

Tayari Young Africans imefanya mazoezi yake ya kwanza nchini Tunisia, baada ya kuwasili mjini Tunis jana jioni kwa saa za Tanzania.

PICHA: Young Africans yaanza mazoezi Tunisia
Mwamnyeto: Ni ngumu kupata ushindi ugenini