Kikosi cha Young Africans rasmi kimeanza mazoezi nchini Tunisia, baada ya kuwasili mjini Tunis jana Jumatano (Februari 08), kikitokea Dar es salaam-Tanzania.

Kurasa za Mitandao ya Kijamii za Young Africans zimethibitisha taarifa za kuanza kwa maandalizi ya kikosi cha klabu hiyo, kwa kuweka picha za Wachezaji wakiwa Uwanja wa mazoezi.

Picha za mazoezi ya wachezaji ya Young Africans imeambatana na ujumbe unaosomeka: “Tumeanza mazoezi rasmi kuelekea mchezo wetu wa kwanza #cafconfederationcup ugenini dhidi ya US Monastir Jumapili”

Serikali kuendeleza udhibiti matumizi mabaya mali ya umma
Fiston Mayele anaitaka GAME na US Monastir