Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, John Heche amelishangaa Bunge kwa kutowapambania wastaafu juu ya kikokotoo cha mafao yao, ambayo yamekuwa yakikanganya kimahesabu na kucheleweshwa kwa malipo, huku akisema Wabunge ni walafi na wachoyo.

Heche ameyasema hayo mbele ya Waandishi wa Habari hii leo Februari 12, 2013 jijini Dodoma, na kusema Serikali iwaache Wastaafu wajipangie matumizi ya fedha zao na si kuwapa kidogo kidogo pindi wanapostaafu, kwani haiwasaidii kufikia malengo waliyojiwekea maishani na Wabunge walipaswa kulisemea jambo hili.

Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama cha Demokwasia na Maendeleo – CHADEMA, John Heche.

Amesema, “ wapo kimya walipaswa kusimamisha Bunge, Wabunge ni walafi na wachoyo, wanazunguka na viti tu pale bungeni na mwishowe wao wakistaafu wanapata zaidi ya milioni mia mbili na hamsini hawasemi kitu wamenyamaza hawaibani Serikali na hii ni hatari kwa Taifa maana wastaafu wanakata tamaa wao wanapata zote na madhara yake ni makubwa baadaye.”

“Wale watu ambao wapo kazini hivi sasa watashindwa kuvumilia, ufisadi utaongezeka watu wataiba ili wajiandae na ustaafu na hasara itaongezeka maana watajiuliza kama hawa wastaafu wanateseka hivi sisi je, na Serikali inasemaje haina hela hivi Serikali huwa unafilisika,” amefafanua Heche.

CHADEMA walia na Serikali kanuni kikokotoo cha mafao
Mikoa hii kunufaika na meli ya MV Mwanza