Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka Watumishi wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuwa waadilifu na wenye kutenda haki, wakati wa kuwahudumia wananchi wanaofika kupima vinasaba.

Waziri Ummy, amesema hayo wakati alipofanya ziaara ya kikazi na kuzindua jengo la ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, na kuongea na Watumishi katika ofisi hizo zilizopo Jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu katika uzinduzi wa jengo la ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikal.

Amesema, “Kazi yenu hii inauhusiano wa karibu na mambo ya kutenda haki, na mimi kwasababu ni mwanamke, kwahiyo katika swala la kuchunguza uhalali wa baba wa mtoto ni yupi napenda sana tuwe waadilifu ili kutenda haki ya kweli bila kuonea yoyote.”

Aidha, Waziri Ummy pia ameelekeza Taasisi zote za umma na binafsi kuweka utaratibu wa kufanya mazoezi, kama sehemu ya mkakati wa Serikali wa kupambana na magonjwa yasiyoambukiza, ikiwemo kisukari na saratani.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 12, 2023
Watakiwa kuungana huduma bora za afya ngazi ya jamii