Inaarifiwa kuwa, katika uchaguzi wa ujao nchini Gabon, hakutakuwa na waangalizi wa Umoja wa Ulaya (EU), ikiwa ni ishara ya wasiwasi kwa upinzani na mvutano uliopo baina ya vyama vya siasa.
Uchaguzi huo wa Urais, Wabunge na Serikali za mitaa unatarajia kufanyika ndani ya mwaka huu (2023), lakini maafisa wa EU walitangaza kuwa hawatatuma timu za kufuatilia mchakato wa upigaji kura.
Hata hivyo, washirika wa karibu na utawala wa Gabon wanasema mzozo wa kidiplomasia wa mwaka 2016 umeacha makovu hata leo na ukisababisha sintofahamu ya nchi waangalizi.
Kwa upande wao, wapinzani wa kisiasa wanaamini kuwa hakuna shirika lingine la kimataifa linaloweza kutuma ujumbe wa uchunguzi, unaoaminika kama ule wa Umoja w Ulaya, EU.