Raia wanaodaiwa kuwa na hasira kali, wamevamia kituo cha Polisi nchini Pakistan kisha kumkamata mfungwa mmoja, Muhammad Waris aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka ya kukufuru, kumtoa nje na kumnyonga.

Tukio hilo, linadaiwa kutokea eneo la Nankana Sahib lililopo mji wa mbali katika jimbo la Punjab lenye idadi kubwa ya watu katika nchi hiyo yenye Waislamu wengi.

Waandamanaji nchini Pakistan katika moja ya matukio. Picha ya NDTV.com

Polisi wa eneo hilo wamesema Waris aliswekwa mbaroni kwa madai ya kuidharau Quran kitu ambacho kiliiwakasirisha wakazi hao waliozunguka kituo cha Polisi, wakitaka mshukiwa huyo akabidhiwe kwao.

Kutokana na umati mkubwa uliokuwa nje ya kituo, Maafisa wa Polisi walikimbia na ndipo Waandamanaji walimkamata mtu huyo na kumburuta hadi barabarani ambako walitimiza azma yao na wamesimamishwa kazi kwa kushindwa kudhibiti tukio hilo.l

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 13, 2023
Hofu ya upinzani: Uchaguzi Mkuu kufanyika bila waangalizi