Polisi Mkoani Iringa, inawashikilia Wafanyakazi wawili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA, Upendo Msigwa (32) na Chali Chaliga (28) kwa tuhuma za kutoa leseni bila kufuata taratibu.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa, Allan Bukumbi amesema Wafanyakazi watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilia.

Katika tukio jingine Polisi imewakamata Omary Kibao (38), Johnson Kihongosi (31), Dickson Nelson(32), baada ya kukutwa na leseni za udereva 31, vitambulisho vya NIDA na Mpiga kura vinne, nakala mbalimbali za kadi za magari na Police loss report.

Aidha, Kamanda Bukumbi amesema watuhumiwa hao walikuwatwa na namba za magari na Pikipiki 431, TIN numbers nane, printer tano, laptop moja na desktop moja, nakala mbili za vyeti vya mafunzo ya udereva, scaner moja na mashine moja ya kulamineti.

Usalama sekta ya Utalii: Polisi wapokea msaada wa Pikipiki
Wananchi Kilombero wamchoma OCD, OC CID