Jeshi la Polisi Mkoani Kagera, linawashikilia watu wanne waliojihusisha na ujangili wa nyara za Serikali katika Hifadhi ya Taifa ya Ibanda Kyerwa na Rumanyika Karagwe.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, William Mwampaghale amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema watuhumiwa wote walikamatwa Februari 13 mwaka huu katika Kijiji cha Muungano, Kata Lusahunga Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.

wataja watuhumiwa waliokamatwa na nyara hizo kuwa ni Raphael Lugaira (44), Fikiri Lugaira  (43), Majaliwa Charles (42) na Warwa Rupily (45), wote wakazi wa Wilaya ya Biharamulo.

Mmoja kati ya walinzi wa wanyama pori nchini Kenya akipanga pembe za Ndovu. Picha ya Reuters.

Kwa mujibu wa Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi, Hifadhi ya Taifa ya Ibanda Kyerwa, Frederick Mofulu alisema walipata taarifa za uwepo wa wahalifu wanaoua wanyama ambapo walishirikisha Jeshi la Polisi na kuwakamata watuhumiwa hao.

Amezitaja nyara zilizokamatwa kuwa ni meno mawili ya tembo, ngozi ya fisi, kichwa cha fisi, vipande vitatu vya ngozi ya nyati, mkia wa nyati na ngozi ya swala na kwamba watuhumiwa hao walikamatwa na silaha mbili aina ya gobole pamoja na risasi tatu za kienyeji aina ya gololi.

Jela maisha kwa kusafirisha dawa za kulevya
Wito wa amani waibua mapigano mapya