Watu wawili wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa baada ya kutokea kwa ajali ya gari kugonga pikipiki mbili barabara ya Moshi -Arusha.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Justine Masejo amesema tukio hilo limetokea februari 15, 2023 baada ya gari lenye namba za usajili T. 493 BJR aina ya Toyota Corona Premio kugongana na pikipiki hiyo iliyokuwa imebeba watu watatu.

Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoani Arusha.

Amewataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Elisha Anthony (25),na Pius Calist Tarimo (17) wote wakazi wa Sokoni one Jijini Arusha na waliojeruhiwa ni Paulo Henry (20) na Saidi Elias (23), ambao kwa pamoja walipatiwa matibabu na kuruhusiwa. 

Kamanda Masejo amewataja majeruhi wengine kuwa ni Emmanuel John (18), na Joshua Fredy Laizer (23) ambao wanaendelea kupatiwa matibu katika Hospitali ya Mount Meru Arusha huku akisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa pikipiki.

Kimbunga: TMA yawatoa hofu Watanzania
Tetemeko laathiri ndoa Uturuki