Kasisi George Olusanya Omoolorun, wa Kanisa la Christ Apostolic Church (CAC) Oke Idahun, Oba-Ile, Akure, amefariki katika mazingira ya utata akiwa mawindoni, baada ya kumpiga risasi mnyama aina ya Kulungu, na kisha kujikuta na jeraha mwilini mwake ambalo lilimsababishia umauti.

Kwa mujibu wa mashuhudia, wamesema tukio hilo limetokea katika eneo la mtaa wa Apeju, Oba-Ile, eneo la Serikali ya Mtaa wa Akure Kaskazini mwa Jimbo la Ondo, ambapo Kasisi huyo alimpiga kulungu huyo risasi lakini wakati akimuwahi Bunduki ilijifyatua na kumjeruhi.

Wamesema, “Kwanza utata unaanzia kwa Kulungu mwenyewe alikuwa na maandishi ya “Ifa” kwenye mwili wake (likiwa na maana ya kifo) na mke wa marehemu alipogundua mumewe hakurudi nyumbani siku hiyo, alimpigia simu lakini ilikuwa ikiita bila majibu.”

Kulungu.

Amesema, “Mke aliogopa na kuwaita dada wa marehemu na majirani wengine ambao walianza kumsaka na walipofika shambani, walikutana naye akiwa hoi chini na kulungu huyo wa ajabu, amesimama kando yake.

“Walikutana naye msituni huku mkono wake ukiwa umeushika sehemu ya jeraha la risasi na walimkuta huyo mnyama Kulungu kando ya Kasisi huyo akiwa hana jeraha lolote na wakamkamata wakati alikuwa akijaribu kutoroka na kugundua ana maandishi ya Ifa kwenye mwili wake.”

Hata hivyo, inasemekana kuwa Kulungu huyo alipelekwa katika kituo cha Polisi cha Oba Ile lakini baadaye alifariki na marehemu lipofikishwa katika Kituo cha afya aliaga Dunia, huku Polisi katika kitengo cha dharula cha Oba-Ile kikithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Mayele atoboa siri ya kuibanjua TP Mazembe
Young Africans warejesha shukurani