Takribani Wauguzi 23, ambapo 18 kati yao wakiwa na asili ya Nigeria wanakabiliwa na mashtaka ya kughushi vyeti vya taaluma za elimu yao katika jimbo la Texas, nchini Marekani .

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya bodi ya wauguzi ya Texas, imesema
wauguzi hao walinaswa katika mpango wa udanganyifu wa stashahada na uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea.

Bodi ya Uuguzi ya Texas ilieleza kuwa, watu waliohusika katika mpango huo walipata vyeti vya udanganyifu vya uuguzi, ambavyo walitumia kufanya mtihani wa bodi ya kitaifa ya uuguzi na tayari imefungua Mashtaka Rasmi dhidi ya wauguzi hao.

Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Idara ya Afya na Huduma za Kibinadamu ya Marekani, ilizinduliwa Januari 25, 2023, ili kuwakamata watu wadanganyifu wenye stashahada na nakala za shahada ya uuguzi.

Robertinho: Uganda itaamua hatma yetu
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 20, 2023