Saa chache kabla ya mtanange wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kati ya Simba SC na wenyeji Vipers SC, Wachezaji wa klabu hiyo ya Tanzania wamepokea nasaha kutoka kwa viongozi walio madarakani na wale wa zamani.
Simba SC itacheza ugenini katika Uwanja wa St Mary’s -Kitende mjini Entebe, ikiwa na lengo la kurekebisha makosa yaliyopelekea kupoteza michezo yao miwili ya awali ya Kundi C, dhidi ya Horoya AC (Guinea) na Raja Casablanca (Morocco).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah ‘Try Again na Mwenyekiti wa Simba SC Murtaza Mangungu wamewaongoza viongozi wengine kukaa chini na wachezaji na kuzungumza nao.
Kubwa lilizongumzwa hapo ni kuwapa moyo wachezaji kwa kuwaaminisha hakuna linaloshindikana katika mchezo wa leo Jumamosi (Februari 25), ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na Mashabiki wa Simba SC.
Viongozi wastaafu walionekana wakitoa Nasaha na Hamasa kwa Wachezaji ni Ismail Aden Rage na Swedy Nkwabi ambao wamewahi kuwa Wenyeviti wa Simba SC kwa vipindi tofauti.
Mwingine ni Hassan Othman Hassanoo, ambaye aliwahi kuwa Makumu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba.