Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amepokea ujumbe wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, ukiongozwa na Rais wake Dkt. Akinwumi Adesina Ikulu, Zanzibar.

Rais Mwinyi akisalimiana na mgeni wake.

Ujumbe huo, umepokelewa hii leo Februari 25, 2023 ambapo Rais Mwinyi ameishukuru Benki ya AfDB kwa kuunga mkono miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo ya kijamii katika sekta ya Afya, barabara, maji na usafiri.

Akiwa na ujumbe huo, Dkt. Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inasimamia sekta zilizo chini ya uchumi wa buluu na kwa upande wa utalii unachangia asilimia 30 ya pato la nchi.

Ujumbe wa AfDB na Rais Dkt. Mwinyi.

Kwa upande wake, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt. Adesina alimuelezea Rais Dk. Mwinyi kuwa miradi ambayo Benki hiyo inasaidia zaidi ni ujenzi wa barabara na sekta ya usafiri ikiwemo ujenzi unaoendelea wa barabara ya Bububu-Mahonda-Mkototoni, barabara ya Tunguu-Makunduchi na ya Mkoani- ChakeChake.

Ajali ya Mtumbwi: Miili ya Wanafunzi wawili yapatikana
PICHA: Viongozi Simba SC wateta na wachezaji