Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua Nehemia Kyando Mchechu kuwa msajili wa Hazina, Mchechu anachukua nafasi ya Mgonya Benedicto ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Rais samia amemteua Hamad Abdallah kuwa Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Nyumba Taifa (NHC), anachukua nafasi ya Mchechu ambaye ameteuliwa kuwa msajili wa Hazina.

Pia, amemteua Mussa Mohammed Makame kuwa Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) kabla ya uteuzi Makame alikuwa mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) na pia ni mshauri mwelekezi wa maswala ya mafuta na gesi nchi, Makame anachukua nafasi ya Dkt. James Mataragio ambaye atapangiwa kazi nyingine.

TAWA yajadili shughuli za uhifadhi pori la akiba
Nabi ashtukia jambo zito Young Africans