Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imekutana na kufanya kikao na viongozi mbalimbali wanaolizunguka Pori la Akiba Kilombero tarehe 23 Februari, 2023, Mkoani Morogoro.

Kikao hiko kililenga kujadili shughuli za uhifadhi wa Pori la Akiba Kilombero na kupanga mikakati ya ushirikiano katika utekelezaji wa Tangazo la Serikali Na. 64 lililoianzisha Pori la Akiba Kilombero.

Tangazo hilo lilitolewa 17 Februari, 2023 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kikao hicho kilijumuisha, Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Mhe. Sebastian Waryuba, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Mhe. Julius Ningu na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Dunstan Kyobya.

Wengine waliohudhuria kikao hiko ni Wakurugenzi wa Wilaya za Mlimba na Ulanga pamoja na Makatibu Tawala wa Wilaya za Ulanga, Malinyi na Kilombero.

TCRA yajadili maboresho uwasilishaji maudhui
Uteuzi: Mchechu ampisha Hamad NHC