Miili ya Wanafunzi wawili,(Ramadhani Nkwila na Tatu Sanari), kati ya wanne waliozama hapo jana Ijumaa Februari 24, 2023 mto Luiche uliopo Mkoani Kigoma wakati wakielekea Shuleni, imepatikana hii leo Februari 25, 2023.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Kigoma, Inspekta Jacob Chacha amesema zoezi la uokoaji liliendelea hii leo na miili hiyo ilionekana ikielea mto Luiche uliopo karibu na Ziwa Tanganyika.

Mtumbwi ziwani. Picha ya Digital DR.

Amesema, miili ambayo bado haijapatikana ni ya Watoto wawili akiwemo Ashura Haruna na Zabibu Jumanne huku akieleza kuwa juhudi za utafutaji zinaendelea ili kuwapata.

Jana Februari 24, 2022 iliripotiwa ajali ya kuzama kwa mtumbwi uliokuwa ukiwavusha wanafunzi hao kuelekea Shuleni, ambapo katika jitihada za uokoaji Watoto Issa Omary darasa la 6 na Michael Logoro wa darasa la kwanza waliokolewa wakiwa hai.

Mke na Mume mikononi mwa Polisi kwa kumchinja mama-mkwe
Dkt. Mwinyi ateta na AfDB ujenzi miradi ya maendeleo