Watuhumiwa wawili wa mauaji ya Bibi kizee (70), wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Geita baada ya kumuuwa kwa kumchinja wakimtuhumu kumuua mtoto wao.

Watuhumiwa hao ni Mtoto wa marehemu Joyce Julius na mumewe Juma Charles ambao kwa pamoja walikuwa wakimtuhumu Bibi huyo kumuuwa mtoto wao usiku wa Februari 23, 2023.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Geita, Berthaneema Mlay amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema upelelezi unaendela ili kuweza kuwfikisha wahusika Mahakamani.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi nchini mara kwa mara limekuwa likikemea vitendo vya kujichukulia maamuzi mikononi na kusisitiza juu ya Jamii kujizoesha kuripoti matukio ya uvunjifu wa amani na kufuata sheria.

Ndejembi ataka kasi utatuzi changamoto za Wananchi
Ajali ya Mtumbwi: Miili ya Wanafunzi wawili yapatikana