Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakuu wa Idara wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, kukerwa na matatizo ya wananchi, kutatua kwa wakati changamoto zao, kupatikana kwa urahisi ofisini na kuondoa urasimu katika utendaji wao wa kazi.

Ndejembi ameyasema hayo hii leo Februari 25, 2023 Jijini Dodoma wakati akifunga kikao kazi cha siku tatu cha Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakuu wa Idara katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi.

Amesema, anawataka watumishi hao kujenga tabia ya kusikiliza na kutolea ufafanuzi matatizo ya wananchi na wasisubiri mpaka taarifa ziwafikie viongozi wa juu, wakati nao wana uwezo wa kuyatatua na kuyatolewa majawabu.

“Sio lazima viongozi wa juu ndio watolee ufafanuzi malalamiko ya wananchi wakati nyinyi mpo na mnawajibu wa kufanya hivyo kabla hayajafika mbali na imani yangu ni kwamba mtakwenda kuyatumia mafunzo haya katika kutatua changamoto za wananchi,” amesema Ndejembi.

Baadhi ya Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakuu wa Idara katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wakimsikiliza Naibu Waziri, Deo Ndejembi. (Hayupo pichani).

Aidha, Ndejembi amewaagiza watendaji hao kusimamia nidhamu ya watumishi kwa kuzingatia sheria za maadili ya utumishi wa umma na kutenda haki, wakati wa kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi.

Trump lazima afe: Brigedia Jenerali Hajizadeh
Mke na Mume mikononi mwa Polisi kwa kumchinja mama-mkwe