Mahakama ya Umma – Peoples Court, ambayo inatajwa kutokuwa na nguvu za kisheria, imemkuta na hatia Rais wa Urusi, Vladimir Putin kwa makosa ya uhalifu wa kivita, dhidi ya Ukraine na kutaka akamatwe.

Uamuzi huo usio na nguvu zozote, umetolewa Februari 24, 2023 wakati ulimwengu ukiadhimisha mwaka mmoja tangu nchi hiyo ya Urusi ilipoivamia Ukraine kijeshi.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin. Picha ya ABC News.

Uamuzi huo, ulifikiwa katika vikao vya Mahakama hiyo vilivyofanyika wiki nzima mjini The Hague, na kusimamiwa na jopo la wataalam watatu wenye uzoefu katika sheria za kimataifa.

Katika maamuzi hayo, waliitaka Jumuiya ya kimataifa kuchukua kila hatua kuhakikisha Mahakama yenye nguvu kisheria kutoa oda ya kumkamata Rais Vladimir Putin, pamoja na kuwachukulia hatua washirika wake.

Mgombea auawa, uchaguzi wasimamishwa
Abdi Banda aishauri Simba SC Ligi ya Mabingwa