Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi nchini Nigeria – INEC, Mahmood Yakubu amesimamisha uchaguzi wa Seneti katika jimbo la kusini mashariki la Enugu, eneo ambalo mgombea wa chama cha upinzani cha Labour aliuwawa.

Akithibitisha sitisho hilo mbele ya waandishi wa Habari, Yakubu amesema “hakutakuwa na uchaguzi wa seneti huko Enugu katika Wilaya ya mashariki kutokana na kifo cha mmoja wa Wagombea hadi pale itakapotangazwa tena.”

Zoezi la upigaji kura nchini Nigeria. Picha ya Financial Times.

Polisi jimbo hilo, imesema mgombea wa chama cha upinzani na dereva wa basi dogo la kampeni waliuawa katika shambulizi lililoratibiwa katika Jimbo la Enugu Februari 23, 2023, kabla ya uchaguzi hii leo Februari 25, 2023.

Ukosefu wa usalama ulioenea nchini humo, umeleta wasiwasi kwa wapiga kura ambao watawachagua wabunge wapya na rais ambaye atachukua nafasi ya Muhammadu Buhari, ambaye haruhusiwi kugombea tena baada ya kuhudumu kwa miaka minane.

Nchi 15 Afrika zagomea kura ya UN kwa Urusi
Uvamizi Ukraine: Mahakama yataka Putin akamatwe