Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Brigedia Jenerali Hosea Ndagala amefanya ziara ya kutembelea Wilaya ya Kigamboni kata ya Mjimwema Mtaa wa Maweni kwa lengo la kuangalia madhara yaliyotokea kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika kikao cha pamoja na Katibu Tawala Msaidizi (Mipango na Uratibu), Chillah Moses katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwaajili ya kupata taarifa kuhusu hali halisi ya madhara ya mvua hizo kwa Wilaya ya Kigamboni alielezwa kuwa maeneo yaliyoathiriwa ni pamoja na Mtaa wa Maweni eneo la Bondeni kata ya Mji Mwema pamoja na Maweni eneo la Biasi ambayo yamezingirwa na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo.

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, itaendelea kuratibu masuala ya menejimenti ya maafa nchini ili kuhakikisha jamii inaendelea kuwa salama na stahimilivu dhidi ya maafa.

Washindi 'Twenzetu Dubai na Parimatch' kwenda Dubai J3
Jaribio la kumuuwa Zelensky laondoka na Mkuu wa Usalama