Kufuatia jaribio la Maafisa wawili katika idara ya ulinzi wa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy kukamatwa wiki hii wakidaiwa kutaka kujaribu kumuua Rais huyo, Mkuu wa Idara ya Usalama, Sergiy Leonidovich Rud amefutwa kazi.

Zelenskiy ametoa amri ya kumfuta kazi Sergiy bila kutaja sababu ya hatua hiyo na bado haiojafahamika ni nani atakayerithi nafasi hiyo muhimu.

Mapema hivi karibuni, idara ya usalama ya Ukraine – SBU, ilisema imezima jaribio la Urusi la kumuua Zelenskiy na maafisa wengine waandamizi serikalini.

SBU iliongeza kuwa inawashikilia makanali wawili inaowashuku walivujisha taarifa kwa shirika la usalama la Urusi FSB, huku taifa hilo likiendelea kushambuliwa na Urusi kwa kutumia ndege za Droni usiku kucha.

Menejimenti ya maafa yatembelea maeneo athiriwa Kigamboni
Athari Kimbunga Hidaya: Urejeshaji huduma za kijamii waendelea