Serikali imetangaza majina ya vijana 812 waliochaguliwa kujiunga katika program ya Building Better Tomorrow, Youth initiative in Agribusiness (BBT-YIA) ambapo Rais Samia anatarajiwa kuzidua shamba lenye ekari 1,000 lililopo jijini Dodoma Machi 20, 2023.
Hayo yamesema na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akizungmuza na waandishi wa habari ambapo amesema mafunzo hayo yamepangwa kuanza Machi 17 na yakuwa ya miezi nne.
Waziri Bashe amesema kati ya hao waliochaguliwa wanawake ni 282,sawa na asilimia 34.73 na wanaume ni 530 sawa na asilimia 65.27 ya waliochaguliwa.
Amesema katika maombi hayo mkoa wa Dar es salaam umeongoza kwa kuwa na waombaji 2,931 sawa na asilimia 14.49 ya maombi yote,huku mkoa wenye waombaji wachache ni Lindi ambapo jumla ya maombi ni 109 sawa na asilimia 0.54.
Bashe amesema kwa upande wa halmashauri ya jiji la Dodoma,limeongoza kwa kuwa na waombaji wapatao 1,800 sawa na asilimia 8.89 ya maombi yote na halmashauri yenye waombaji wachache ni Nyasa
Aidha ameeleza kuwa katika programu hii serikali itawawezesha vijana kushiriki Kilimo biashara kupitia mashamba ya pamoja.