Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally ameanza Kampeni za kuelekea michezo miwili ya nyumbani ya Kundi C, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika itakayochezwa Machi 07 na 18.

Simba SC itacheza dhidi ya Vipers SC ya Uganda katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku ikihitaji matokeo yatakayowapa alama tatu, ili kuendelea kuongeza matumaini ya kufuzu Robo Fainali ya Michuano hiyo ya Afrika msimu huu 2022/23.

Baada ya mchezo huo Simba SC itaendelea kuwa nyumbani kwa kupambana na Horoya AC kutoka nchini Guinea, na kama mambo yatawanyookea kwa kupata alama tatu kwenye mpambano huo, watafikisha alama 09.

Kutokana na umuhimu wa michezo hiyo, Ahmed Ally anaamini mtaji pekee wa ushindi ambao huenda ukatimiza malengo yao msimu huu, ni Mashabiki wa Simba SC ambao wanapaswa kwenda Uwanja wa Benjamin Mkapa kuishangilia timu yao itakapokuwa na kibarua cha kuziwania alama 06.

Ahmed Ally ametumia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii kuanza kuhamashisha Mashabiki wa Simba SC, ili kutimiza malengo waliojiwekea kuelekea michezo hiyo miwili ambayo ni muhimu sana kwa Klabu yao kushinda.

Ahmed ameandika: Asante Mungu Ushindi wetu wa Uganda ni ishara kuwa kazi ya kuitafuta robo fainali inaanza.

Haitakua rahisi maana Vipers hatakubali kufungwa nje ndani na Horoya hatakubali kupoteza matumaini yake.

Lakini yote yanawezekana kama kila Mwana Simba atatimiza majukumu yake.

Agenda kuu ya Kitaifa ya Wana Simba hivi sasa ni ?????????? ? ?????? ??? ?? ??? ??????? ????? (Mpango ni alama 6 Jicho kwenye Robo Fainali).

Kila mwenye silaha, Mwenye mawazo na mwenye mbinu atumie ili azma yetu itimie
Kwa mashabiki wenzangu tuanze sasa maandalizi ya March 7, Jukumu letu ni kuujaza Uwanja na kushangilia.

Sababu za Baleke, Bocco , Sakho kuwekwa benchi
Musonda: Tulistahili tulichokipata