Serikali nchini, inatarajia kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja hadi Saudi Arabia ambapo safari ya kwanza kati ya Dar es Salaam na Jeddah, inatarajiwa kuanza tarehe 26 Machi 2023.

Hayo yamebainishwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Ali Mwadini na Meneja Mkuu wa Masoko Kanda ya Kati wa Shirika la Ndege la Saudi Arabia, Abdulrahman Alabdulwahab.

Viongozi hao, pia wamejadili maandalizi ya uzinduzi wa safari za ndege za moja kwa moja kati ya Tanzania na Saudi Arabia na mikakati ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania, ili kuongeza idadi ya watalii na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa za Tanzania hususan nyama na matunda.

Prof. Nombo ataka kasi kuinua sekta ya elimu
Mapenzi, ushirikina chanzo matukio ya mauaji Kagera